Azimio kuhusu hali ya amani na usalama kwenye eneo la Sahara


African Union

Azimio kuhusu hali ya amani na usalama kwenye eneo la Sahara

BUNGE LA AFRIKA,LIKIZINGATIA Ibara ya 17 ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika, ulioanzisha Bunge la Afrika ili kuhakikisha ushiriki kikamilifu wa watu wa Afrika katika maendeleo na utangamano wa kiuchumi wa bara;LIKIZINGATIA PIA Ibara ya 3(a), (f) na (k) ya Mkataba Anzilishi wa Umoja wa Afrika inayoelezea malengo ya Umoja wa Afrika ili kuwa na umoja na mshikamano mkubwa miongoni mwa nchi za Afrika na watu wa Afrika, kukuza amani, usalama, na utulivu katika bara; kukuza ushirikiano katika nyanja zote za shughuli za binadamu ili kuboresha viwango vya maisha vya watu wa Afrika.LIKIZINGATIA ZAIDI Ibara ya 3 ya Protokali ya Mkataba Anzilishi wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika inayohusiana na Bunge la Afrika, ambayo inawezesha utekelezaji kikamilifu wa sera na malengo ya Umoja wa Afrika; kukuza kanuni za haki za binadamu na demokrasia barani Afrika, na kukuza amani, usalama na utulivu.LIKIREJEA Ibara ya 20 ya Mkataba Anzilishi ambayo pia inarejewa kwenye Ibara 9 ya Protokali ya Marekebisho ya Mkataba Anzilishi ya mwaka 2003; na Ibara ya 2 ya Protokali ya mwaka 2002 inayohusiana na Uanzishwaji wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kama "chombo kinachosimamia uamuzi wa kuzuia, kusimamia na kutatua migogoro.LIKIREJEA Lengo la 4 la Ajenda 2063 ambalo linalenga kuwa na Muundo wa Amani na Usalama unaofanya kazi kikamilifu barani Afrika (APSA) kwa ajili ya kulinda amani, usalama na utulivu barani Afrika.LIKIZINGATIA kwamba mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kubwa zinazolikabili eneo la Sahara ambapo karibu asilimia 80 ya maeneo ya kilimo katika eneo la Sahara yameathirika na mabadiliko ya tabianchi hivyo kuathiri shughuli za kujiingizia kipato kwa watu wa eneo hilo;LIKITAMBUA KWA MASIKITIKO kwamba kuongezeka kwa joto kwenye eneo la Sahara ni zaidi ya mara moja na nusu kuliko wastani wa dunia jambo ambalo limekuwa na athari kubwa kwenye upatikanji wa maji katika eneo la Sahara na kusababisha eneo hilo ambalo ni nusu jangwa kukabiliwa na changamoto kubwa za kudumu ikiwa ni pamoja na madhara makubwa ya mabadiliko ya tabianchi, mvua zisizotabirika, ukame wa mara kwa mara ambao umesababisha kupungua kwa mavuno na rasilimali ya maji kutokana na viwango vya juu vya joto katika eneo hilo ambavyo vinaathari mazingira;LIKITAMBUA pia KWA MASIKITIKO kwamba ugaidi na siasa kali vinaendelea kuchochea kusambaa kwa silaha haramu ndogo ndogo ambazo zinatishia amani na usalama barani Afrika na kukwamisha juhudi za kuboresha hali za maisha ya watu wa Afrika;LIKITAMBUA PIA kwamba sababu tofauti zinachangia uhamiaji haramu, usafirishaji haramu wa binadamu na mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara yanayofanywa na AQIM na Boko Haram na makundi mengine ya kigaidi katika eneo la Sahara;LIKITAMBUA ZAIDI kiwango cha silaha ndogo ndogo zinazosambaa katika eneo la Sahara; na madhara yake kwa amani na usalama kutokana na kuzuka kwa mapigano ya mara kwa mara, vitendo vya kigaidi na siasa kali barani;LIKIRIDHISHWA na juhudi zinazofanywa na serikali kwenye eneo la SAHARA na jukumu linalotekelezwa na Baraza la Amani na Usalama katika Kanda hiyo;KWA MUJIBU WA ya Kanuni 5 (b), (c) na (d) ya Kanuni za Uendeshaji wa Bunge la Afrika, ambayo pamoja na mambo mengine, inalipa BA madaraka ya kuandaa mijadala, kujadili, kutoa maoni, kutoa mapendekezo kuhusiana na malengo na jambo lolote linalohusiana na Umoja wa Afrika na vyombo vyake, Jumuiya za Uchumi za Kanda, Nchi Wanachama na vyombo na taasisi zake;
SASA LINAAZIMIA:Kuunda tume ya kutafuta ukweli wa mambo kwenda eneo la SAHARA ili kutathmini wakimbizi na hali ya kibinadamu kwenye eneo hilo na athari zake kwa amani, usalama na utulivu kwenye eneo hilo.Limepitishwa Midrand, Afrika Kusini17 Oktoba 2019
▲ To the top